Jumatatu 25 Mei 2026 - 06:38
Harakati ya Wananchi wa Iraq yatoa onyo kuhusu njama za Jordan

Hawza/ Hussein Al-Karawi ameonya kuhusu njama iliyoanzia Jordan, ambayo lengo lake ni kuibua mifarakano na mgawanyiko ili kuiweka serikali ya Iraq katika mzozo na wana wa Muqawama.

Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Hussein Al-Karawi, mkuu wa kamati ya uratibu ya Harakati ya Wananchi wa Iraq, ameonya kuhusu njama iliyoanzia Jordan, ambayo lengo lake ni kuibua mifarakano na mgawanyiko kwa nia ya kuiweka serikali ya Iraq katika makabiliano na wana wa Muqawama.

Al-Karawi alisema katika mazungumzo yake na chombo cha habari cha Al-Maaloumah: “Upande wa Marekani, utawala wa Kizayuni na washirika wao katika eneo hili, baada ya kushindwa walikokumbana nako katika vita vya hivi karibuni, wamekuwa dhaifu na wasioweza kukabiliana na Mhimili wa Muqawama.”

Aliongeza kuwa: “Mhimili wa Muqawama unaiona Jordan kuwa uwanja wa mbele wa kukiuka mamlaka na uhuru wa Iraq na kuwalenga wana wa Muqawama kutoka katika ardhi ya nchi hiyo, kwa ajili ya kuhudumia mradi wa Kizayuni na Amerika na maslahi yao nchini Iraq na katika eneo lote.”

Al-Karawi alisisitiza kuwa: “Jordan si tu imetumika kama ardhi ya kuishambulia Iraq na kuwalenga wana wa Muqawama, bali pia ni kituo ambacho njama zote za kuleta mifarakano na mgawanyiko ndani ya Iraq zinatokea na kuanzia humo, hatua hii ni jaribio la kuiweka serikali ya Iraq katika makabiliano na wana wa Mhimili wa Muqawama ambao wamesimama pamoja na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha